Wawa aitaka Fainali Shirikisho Afrika

Mlinzi wa kati Pascal Wawa amefunguka kuwa timu itahakikisha tunapambana katika mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Orlando Pirates kupata matokeo mazuri kwa kuwa lengo ni kufika fainali ya michuano hii.

Wawa ameweka wazi kuwa mchezo huo utakaopigwa Jumapili nchini Afrika Kusini utakuwa mgumu kwa kuwa wenyeji Orlando watataka kupindua matokeo lakini tupo tayari kuhakikisha tunawazuia.

Mkongwe huyo pia amewashukuru mashabiki wetu waliojitokeza kwa wingi katika mchezo wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Jumapili iliyopita kuwa walitupa nguvu mpaka kuibuka na ushindi.

“Kama nilivyowahi kusema awali lengo sio kufika nusu fainali pekee bali tunahitaji kuvuka na kufika fainali. Tunamtanguliza Mungu atuongoze kwenye hili nasi wachezaji tutapambana kufanikisha.

“Tunafahamu mchezo wa marudiano utakuwa mgumu, Orlando watataka kupindua matokeo lakini tumejipanga kuhakikisha tunawazuia ili tupate nafasi ya kusonga mbele,” amesema Wawa.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER