Alichosema Matola kuelekea mchezo wa kesho wa Fainali dhidi ya Azam

Kocha Msaidizi, Seleman Matola amesema mchezo wa kesho wa fainali ya michuano ya Kombe la Muungano dhidi ya Azam FC utakuwa mgumu kutokana na kukutanisha timu bora.

Matola amesema mara zote tunapokutana na Azam mchezo unakuwa mgumu na huu ni mchezo wa fainali kwahiyo tumejiandaa kuhakikisha tunafanya vizuri.

Matola ameongeza kuwa kikosi kipo kwenye hali nzuri na wachezaji wamejipanga kuhakikisha tunapata ushindi na kuibuka Mabingwa wa michuano hii.

“Itakuwa mechi ngumu, Azam ni timu bora lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda. Hii ni fainali na siku zote haiwezi kuwa nyepesi kwahiyo tumejipanga kuwakabili,” amesema Matola.

Kwa upande wake nahodha msaidizi Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amesema wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho ingawa amekiri utakuwa mgumu.

“Utakuwa mchezo mgumu, tunaiheshimu Azam lakini tupo tayari na tutaingia uwanjani kwa lengo la kutafuta ushindi ili tuibuke na ushindi,” amesema Zimbwe Jr.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER