Alichosema kocha Mgunda baada ya ushindi dhidi ya Yanga

Kocha Mkuu wa Simba Queens Juma Mgunda amesema licha ya ushindi wa mabao 3-1 tuliopata dhidi ya Yanga Princess lakini haikuwa mechi rahisi.

Mgunda amesema tukigemea kupata upinzani mkubwa kutoka Yanga hasa tukizingatia tuliwafunga katika mchezo wa mzunguko wa kwanza.

Mgunda amesema ilibidi tutumie madhaifu ya Yanga kipindi cha pili ili kupata mabao baada ya kuwasoma vizuri.

“Ligi ni ngumu, kila timu imejipanga vizuri, Tulitegemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Yanga lakini tulikuwa bora zaidi,” amesema Mgunda.

Akizungumzia mchezo unaofuata dhidi ya JKT Queens, Mgunda amesema “itakuwa mechi ngumu lakini tutajiandaa kuwakabili.”

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER