Queens yaichakaza Yanga Princess

Timu yetu ya Simba Queens imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Yanga Princess katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania (TWPL) uliopigwa Uwanja wa Azam Complex.

Mchezo huo ulianza kwa kasi huku timu zote zikishambuliana kwa zamu na umiliki wa mpira ukiwa sawa katika muda mwingi wa kipindi cha kwanza.

Aisha Juma alitupatia bao la kwanza dakika ya 51 baada ya Kupokea Pasi Nzuri Kutoka Kwa Vivian Corazone.

Dakika Ya 66 Jentrix Shikangwa alitupatia goli la pili kwa shuti kali lilomshinda mlinda mlango wa Yanga Princess, Belina Nyamwihula baada ya makosa ya safu yao ya ulinzi.

Aisha Juma alitupatia bao tatu kwa shuti kali nje ya 18 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Joanitah Ainembabazi na kumshinda mlinda mlango wa Yanga.

Kaeda Wilson aliwafungia Yanga Princess bao la dakika ya 94 kwa shuti kali lililomshinda mlinda mlango wetu Carorlyne Rufa

Kocha Juma Mgunda alifanya mabadiliko ya kuwatoa Danai Bhobo, Jentrix Shikangwa, Daniela Ngoyi, Eliza Wambui na kuwaingiza Ritticia Nabbosa, Joanitah Ainembabazi, Ester Mayala na Olaiya Barakat.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER