Timu yawasili Singida

Kikosi chetu kimewasili salama mkoani Singida kutoka Kigoma kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC unaofuata dhidi ya Ihefu FC.

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu, Ahmed Ally amesema kwa sasa nguvu zetu tunazielekeza kwenye Ligi Kuu baada ya kutolewa kwenye michuano yote.

Ahmed amesema tunahitaji kushikamana katika kipindi hiki nakuwa pamoja ili tuweze kupata taji hili moja ambalo ndilo pekee tunalolipigania.

Akizungumzia hali ya kikosi Ahmed amesema wachezaji wapo kwenye hali nzuri ambapo hata mlinzi Henock Inonga ambaye aliukosa mchezo wa jana anaendelea vizuri na anaweza kuwepo kwenye kikosi kitakachocheza dhidi ya Ihefu.

“Kikosi kimeondoka saa nne asubuhi mkoani Kigoma na kimewasili usiku huu tayari kwa mchezo huo ambao utapigwa katika Uwanja wa Liti Jumamosi saa 10 jioni.”

“Timu itapata siku mbili ya kufanya mazoezi ikiwa hapa Singida yaani kesho Alhamisi na Ijumaa kabla ya kushuka dimbani Jumamosi,” amesema Ahmed.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER