Kaimu Kocha Mkuu, Juma Mgunda tayari amejiunga na kikosi na jioni hii ameiongoza timu kwenye mazoezi ya mwisho yaliyofanyika Uwanja wa Majaliwa kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Namungo.
Mgunda amejiunga na timu na ameiongoza kwenye mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Namungo ambao utapigwa katika uwanja huo huo saa 12 jioni.
Wachezaji wote 20 tuliosafiri nao wameshiriki mazoezi hayo na wapo kwenye hali nzuri kuelekea mchezo wa kesho na lengo letu ni kuhakikisha tunashinda.
Mgunda anachukua nafasi ya Abdelhak Benchikha ambaye ameomba kuvunja mkataba kutokana na matatizo ya kifamilia.
Mgunda atasaidiana na Seleman Matola kuiongoza timu katika kipindi hiki mpaka Bodi ya Wakurugenzi watakavyoamua tofauti.