Queens yazidi kupaa TWPL

Timu yetu ya Simba Queens imezidi kujikita kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Wanawake (TWPL) baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Tanzania mtanange uliopigwa Uwanja wa Azam Complex.

Aisha Mnuka alitupatia bao la kwanza dakika ya tano baada ya kumalizia pasi safi iliyopigwa na Jentrix Shikangwa kutoka upande wa kulia.

Baada ya bao hilo timu zote ziliendelea kushambuliana kwa zamu lakini safu za ulinzi zulikuwa imara kuzuia mashambulizi.

Mlinzi wa kati Ruth Ingosi alitupatia bao la pili dakika ya 61 kwa shuti kali la mguu wa kushoto baada ya kumzidi ujanja mlinzi wa JKT Queens.

Baada ya bao hilo JKT waliongeza kasi na kufanya mashambulizi lakini safu yetu ya ulinzi ilikuwa imara kuwadhibti.

Matokeo haya yanatufanya kufikisha pointi 37 alama tisa juu ya JKT Queens walionafasi ya pili baada ya kucheza mechi 13.

Kocha wa Queens Mussa Hassan Mgosi alifanya mabadiliko ya kuwatoa Jentrix Shikangwa, Fatuma Issa, Asha Rashid, Ritticia Nabbosa na Elizabeth Wambui na kuwaingiza Diana Mnaly, Joanitah Ainembabazi, Ester Mayala na Danai Bhobho.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER