Simba yajipima na Cambiaso mbele ya Pablo

Kocha Mkuu Pablo Franco, leo ameshuhudia mchezo wa kirafiki wa kimazoezi dhidi ya Cambiaso Sports uliopigwa saa 10 jioni katika Uwanja wa Boko Veterans na kumalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Mechi hiyo ilianza kwa kasi huku timu zikishambuliana kwa zamu zikionekana kutaka kutafuta bao la mapema ingawa tulitawala sehemu kubwa ya mchezo.

Mchezo huo ni wa kwanza kwa Kocha Pablo ambaye alianza jana kukinoa kikosi chetu na alihitaji mechi ya kirafiki ili kuona aina ya uchezaji wetu.

Mabao yetu yalifungwa yote kipindi cha kwanza kupitia kwa Joseph Mbaga dakika ya 20 kabla ya Hassan Dilunga kuongeza la pili kwa mkwaju wa penati dakika ya 41.

Kipindi cha pili Cambiaso waliongeza kasi ya mashambulizi langoni kwetu na kufanikiwa kusawazisha mabao yote dakika za 64 na 68.

Kocha Pablo aliwatoa Kakolanya, Gadiel, Mbaga na Katerego na kuwaingiza Kisubi, Saad Mwaipopo na Katerego.

Kikosi Kamili kilivvyokuwa

Beno Kakolanya, Issa, Gadiel Michael, AbdulSamad Kassim, Pascal Wawa, Jonas Mkude, Jimson Mwinuke, Yusuph Mhilu, Ibrahim Ajibu, Hassan Dilunga na Josephat.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER