Simba Sports Club

Wambui kuikosa michuano ya CECAFA Qualifiers

21 Aug 2026

Kiungo wetu mshambuliaji wa Simba Queens, Elizabeth Wambui ataikosa michuano ya ya CAF Womens Champions League CECAFA Qualifiers 2026 inayofanyika Kigali Rwanda baada ya kuumia mguu wa kulia.

Maumivu hayo aliyapata tukiwa nchini Kenya tulipokuwa tumeweka kambi ya maandalizi kabla ya kufika hapa Kigali Rwanda kwa ajili ya michuano hiyo.

Baada ya kupata majeraha hayo jopo la Madaktari lilifanya maamuzi ya nyota huyo kubaki Kenya kwa ajili ya matibabu zaidi ikingizatiwa kuwa ndipo nyumbani kwao.

Advertisement

Elizabeth alianza kupata matibabu ya haraka chini ya Daktari wa timu, Fatuma Omary na majibu ya awali yameonyesha atakuwa nje ya uwanja kwa wiki mbili.

“Tunaenda kwenye mashindano bila ya Elizabeth ila tupo nae karibu kwa uangalizi mkubwa na matibabu ya awali yameonyesha atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki mbili baada ya hapo tutamfanyia vipimo zaidi ili kujua ukubwa wa tatuzo,” amesema Dkt.Fatuma.

Kabla ya kuanza safari ya kuelekea Rwanda wachezaji, benchi la ufundi na Viongozi walimuaga Elizabeth na kumuombea apone haraka.