Tumefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Pamba Jiji katika mchezo wetu wa pili wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Clatous Chama alitupatia bao la kwanza dakika ya 17 baada ya mpira wa adhabu uliopigwa na Libasse Gueye kuokolewa na mlinda mlango, Eric Johola kabla ya kumkuta mfungaji.
Anicet Oura alitupatia bao la pili kwa kichwa dakika ya 30 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Libasse Gueye.
Kiungo mkabaji, Ibrahim Jabaar alitolewa nje kwa kuonyeshwa nyekundu ya moja kwa moja dakika ya 44 baada ya kumpiga kiwiko mshambuliaji, Abdulkarim Issa.
Pamba Jiji ilipata bao la kwanza kwa mkwaju wa penati dakika ya 72 kupitia Idris Diomande baada ya kiungo Daud Semfuko kumfanyia madhambi Yonta Camara ndani ya 18.
Matokeo haya yanatufanya kufikisha alama sita baada ya kucheza mechi mbili tukifunga mabao manne na kuruhusu moja pekee.
Mchezo wetu unaofuata utakuwa dhidi ya Singida Black Stars utakaopigwa Jumamosi Agosti 22 katika Uwanja wa Airtel mkoani Singida.
X1: Erick, Zabona, Ally, Nonyem, Deogratius (Camara 63'), Vellim, John, Shaphan (Kibailo 45') Abdallah, John (Diomande 45'), Abdulkarim (Nata 63')
Walioonyeshwa kadi: Shaphan 14' Nonyem 65' Opondo 81'
X1: Abel, Nathaniel, Mligo, Toure, De Reuck, Maema (Semfuko 61'), Gueye (Makgalwa 67'), Jabaar, Mpanzu (Doumbia 67'), Chama, Oura
Walioonyeshwa kadi: Jabaar kadi nyekundu 44' Makgalwa 90'