Simba Sports Club

Mgosi ana matumaini makubwa na Simba Queens

21 Aug 2026

Kocha mkuu wa Simba Queens, Mussa Hassan ‘Mgosi’ ameweka wazi kuwa ana matumaini ya kufanya vizuri kwenye michuano ya CAF Womens Champions League CECAFA Qualifiers 2026 inayofanyika nchini Rwanda kutokana na maandalizi tuliyofanya.

Mgosi ametoa kauli hiyo zikiwa zimebaki saa chache kabla ya kuivaa Top Girls ya Burundi kwenye mchezo wa kwanza wa mashindano hayo utakaopigwa kesho saa 10 jioni katika Uwanja wa Pele hapa Kigali Rwanda.

Mgosi ameongeza kwa kusema kuwa kulingana na maandalizi tuliyofanya nyumbani Dar es Salaam na baadae Nairobi, Kenya na kupata mechi kadhaa za kirafiki kikosi chetu kimeimarika na kipo tayari kwa mashindano.

“Tumeiandaa timu yetu ili kuonyesha kiwango bora katika kila mchezo uliokuwa mbele yetu ili kupata matokeo mazuri ya ushindi yatakayo tuwezesha kusonga mbele kwenye hatua hii ya makundi," amesema Mgosi.

Advertisement

Wakati huo huo nahodha wa timu, Ester Mayala amesema wachezaji wana morali ya hali na matumaini ya kufanya vizuri ni makubwa kwasababu ya maandalizi mazuri tuliyofanya.

“Morali ipo juu na wachezaji wote tupo tayari kwenda kufanya vizuri katika mechi hii ya kwanza ili kupata ushindi na kujiweka katika mazingira mazuri kutinga hatua inayofuata," amesema Ester.

Simba Queens imepangwa kundi C, pamoja na Kenya Police na Top Girls huku kinara kati timu hizi atafuzu moja kwa moja hatua ya nusu fainali itayotafanyika Agosti 29.