Simba Sports Club

Tutacheza na Polisi Kenya Simba Day

1 Aug 2026

Kwenye kilele cha Tamasha la Simba Day litajalofanyika katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, Agosti 8 tutacheza mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya Polisi Kenya.

Huu ni utaratibu wetu wa kualika timu kutoka nje kucheza nao mechi ya kirafiki kwenye kilele cha Simba Day ili kuwapa fursa mashabiki wetu kuiona timu yao ambayo itashiriki mashindano mbalimbali katika msimu wa 2026/2027.

Advertisement

Tumeichagua timu ya Polisi Kenya ambao ni Mabingwa wa Kenya katika msimu wa 2024/2025 kutokana na ubora walionao na tunaamini watatupa ushindani mkubwa.

Mechi ya kirafiki dhidi ya Polisi Kenya litakuwa tukio la mwisho la Simba Day lakini litatanguliwa na shughuli mbalimbali kama burudani, mechi za kirafiki pamoja na utambulisho wa wachezaji.