Simba Sports Club

Tumezindua Wiki ya Simba Ngorongoro

1 Aug 2026

Leo tumezindua rasmi Wiki ya Simba ikiwa zimebaki siku saba kuelekea Tamasha la Simba Day ambalo litafanyika Agosti, 8 katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam tukio lililofanyika katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro jijini Arusha.

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu, Seleman Haroub pamoja na Mkurugenzi wa Naibu Kamishna wa Uhifadhi huduma za slShirika (NCAA) ndugu Aidan Makala ndio waliiongoza zoezi hizo ambalo lilikuwa na matukio matatu makubwa.

Tukio la kwanza lilikuwa ni uzinduzi wa jezi, la pili kumtangaza Msanii mkuu atakaye tumbuiza siku hiyo pamoja na kutangaza timu ambayo tutacheza nayo mechi ya kirafiki.

Advertisement

Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu, Ahmed Ally amemtangaza nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Ally Saleh Kiba 'King Kiba' kuwa ndiye mtumbuizaji mkuu katika Tamasha hilo.

King Kiba amekuwa akishiriki Matamasha mbalimbali yanayoandaliwa na klabu kutokana na mapenzi makubwa aliyonayo kwa timu yetu.

Mbali na King Kiba pia kutakuwa na Wasanii mbalimbali watakaopamba Simba Day ya mwaka huu ambayo tunatimiza miaka 90 ya kuanzishwa kwa klabu yetu pamoja na burudani mbalimbali.