Simba Sports Club

Tumemaliza Kagame kwa Ushindi

31 Jul 2026

Mchezo wetu wa mwisho wa hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Kagame dhidi ya Singida Black Stars uliopigwa Uwanja wa Amahoro umemalizika kwa ushindi wa mabao 2-1.

Ibrahim Doumbia alitupatia bao la kwanza dakika ya 27 kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Libasse Gueye.

Baada ya bao hilo tuliendelea kushambuliana kwa zamu huku tukiwa tumemiliki sehemu kubwa ya mchezo muda mwingi.

Methew Tegisi aliisawazishia Singida bao hilo dakika ya 49 baada ya kumalizia shuti kali lililopigwa na Shekhan Ibrahim kupanguliwa na mlinda mlango, Djibrilla Kassali.

Elie Mpanzu alitupatia bao la pili dakika ya 66 ikiwa ni dakika moja tangu aingie uwanjani baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na David Kameta 'Duchu'.

Advertisement

Matokeo haya yanatufanya kufikisha pointi tano tukiwa nafasi ya pili alama mbili nyuma ya vinara wa Kundi B Jamus kutoka Sudan Kusini.

X1: Kassali, Duchu, Kibabage (Chilambo 72'), Toure (Masinde 72') De Reuck (Mligo 72') Kagoma (Loemba 75') Gueye (Msimu 65') Chama, Doumbia (Mpanzu 65'), Makgalwa (Jabaar 65') Oura,

Walioonyeshwa kadi: Kassali 90+4'

X1: Yona, Pipino (Omary 61'), Hemedy, Miraji, Mwashinga, Nindi, Canadi (Mtange 61') Nzaou (Chikola 79') Shekhan, Henry (Yusuph 71'), Tegisi (Sowah 79')

Walioonyeshwa kadi: Nindi 32' Tegisi 32' Sowah 90'