Droo ya hatua makundi kwa timu kutoka Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kwa upande wa Wanawake imekamilika Uwanja wa Amahoro Kigali nchini Rwanda.
Simba Queens ni mwakilishi pekee kutoka Tanzania kwasababu ndiye bingwa wa Ligi Kuu msimu uliopita wa 2025/2026.
Simba Queens tumepangwa Kundi C pamoja na timu za Polisi Kenya na Top Girls Academy kutoka Burundi.
Advertisement
Mashindano hayo yataanza kutimua vumbia Agosti 21 na kuhitimika Agosti 31 katika Jiji la Kigali nchini Rwanda.
Bingwa wa michuano hiyo ataiwakilisha CECAFA katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Wanawake ambayo ratiba yake itatangazwa baadae.