Leo saa moja usiku kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi kuikabili Azam FC 'Mzizima Derby' katika mchezo wa sita wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2026/2027.
Mzizima Derby ni moja ya mechi ngumu ambayo mara nyingi imekuwa ikiamuliwa na mbinu za makocha uwanjani kitu ambacho kimekuwa kikiwavutia mashabiki wengi
Nafasi za timu zote kwenye msimamo....
Tupo nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC tukiwa na alama 15 na mabao tisa baada ya kupata ushindi kwenye michezo yote mitano tuliyocheza tukiwa na ushindi wa asilimia 100.
Kwa upande wapinzani wetu Azam FC wapo nafasi ya tatu kwenye msimamo wakiwa na alama 14 baada ya kushinda mechi nne kutoka sare mbili.
Tulivyokutana mara ya mwisho....
Msimu uliopita tulipata alama moja pekee dhidi ya Azam kitu ambacho kinatupa motisha kubwa ya kupambana kuelekea mchezo wa leo.
Mchezo wa kwanza msimu uliopita tuliocheza katika Uwanja wa Benjamin Disemba 7/2025 Mkapa tulipoteza kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Japhte Kitambala na Idd Suleiman 'Nado'.
Mchezo wa mzunguko wa pili uliopigwa Aprili 5/2026 katika Uwanja wa Azam Complex tulitoka sare ya bila kufungana.
Hali ya Kikosi....
Wachezaji wote isipokuwa waliokuwa majeruhi wa muda kama Shomari Kapombe, Nickson Kibabage, Wilson Nangu na Abdulazak Hamza ndio tutawakosa katika mchezo wa kesho.
Wachezaji wengine wote wameshiriki mazoezi ya mwisho jana katika uwanja wa Gymkhana na hakuna aliyepata majeraha ambayo yatamfanya kuukosa mchezo wa leo.
Kwa upande wa Azam Mkuu wake wa kitengo cha Habari na Mawasiliano, Thabit Zakaria 'Zakazakazi' ameweka wazi kikosi chao kipo kamili kwa asilimia 99 ambapo watamkosa mchezaji mmoja pekee ambaye ni majeruhi.
Wachezaji wakuchungwa.....
Libbase Gueye, Anicet Oura, Elie Mpanzu na Clatous Chama ni nyota ambao wanatarajiwa kuwa mwiba mchungu kwa safu ya ulinzi ya Azam kwenye mchezo wa leo.
Kwa upande wa Azam nyota wao wa kuchungwa ni Feisal Salum, Kipre Junior, Idd Nado, Djibril Sillah ambao ndio nyenzo kubwa ya upatikanaji mabao wa 'Matajiri' hao wa Dar es Salaam.
Matarajio ya jinsi mechi itakavyokuwa......
Mchezo unatarajiwa kuwa wakuvutia kutokana na aina ya soka kwa pande zote na mbinu bora pekee ndizo zitafanya timu yoyote kupata alama tatu katika mechi ya leo.