Simba Sports Club

Tumetinga hatua ya pili Mabingwa Afrika Kibabe

13 Sep 2026

Tumefanikiwa kutinga hatua ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 6-1 dhidi ya Mighty Wanderers katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Uhuru

Clatous Chama alitupatia bao la kwanza dakika ya saba kwa shuti kali la mguu wa kushoto akiwa ndani ya 18 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Anicet Oura.

Libbase Gueye alitupatia bao la pili dakika ya 28 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Elie Mpanzu kutoka upande wa kushoto.

Chama alitupatia bao la tatu dakika ya 33 baada ya kumalizia mpira uliookolewa na mlinda mlango wa Might Wanderers, Dalitso Phiri kufuatia shuti kali lililopigwa na Oura.

Isack Kaliati aliipatia Mighty Wanderers bao la kwanza ya 43 kwa mkwaju wa penati baada ya nahodha msaidizi, Rushine De Reuck kumfanyia madhambi mshambuliaji, Clement Nyondo ndani ya 18.

Libbase alitupatia bao la nne dakika ya 69 kwa shuti la mguu wa kushoto tuliomshinda mlinda mlango, Phiri baada ya kupokea pasi kutoka kwa Oura.

Kaletso Makgalwa alitupatia bao la tano dakika 88 baada ya Ismail Mgunda kufanya kazi kubwa ya kutoka na mpira katikati ya uwanja na kutoa pasi safi ya bao.

Advertisement

Morice Abraham alitupatia bao la sita dakika ya mwisho ya kipindi cha pili baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Makgalwa.

Tumetinga hatua hatua hii kwa jumla ya mabao 7-1 kufuatia ushindi wa bao moja tuliopata kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Taifa wa Bingu nchini Malawi.

Matokeo haya yanatufanya kukutana na 15 De Agosto ya Equatorial Guinea ambayo imeitoa Fomboni FC ya Comoro kwenye hatua hii ya awali.

Mechi za kwanza hatua ya pili itapigwa Oktoba 16-18 wakati mechi ya marudiano itakuwa Oktoba 23-25.

X1: Kassali, Chilambo, Mligo, Toure, De Reuck, Kagoma, Gueye (Mgunda 79'), Maema (Jabaar 76'), Mpanzu (Doumbia 63'), Chama (Morice 62'), Oura (Makgalwa 76')

Walioonyeshwa kadi:

X1: Phiri, Singini, Kamwendo, Chirwa, Sanubi, Silwimba, Ng'ambi (Kamanga 33'), Nyirenda (Kudonto 39'), Kaliati (Nahipa 99'), Mithi (Nyondo 38')

Walioonyeshwa kadi: Zulu 18' Silimbwa 79' Thierry 86'