Simba Sports Club

Kauli ya Kocha Barker kuelekea mchezo dhidi ya Azam

15 Sep 2026

Kocha Mkuu Steve Barker amesema wazi kuwa mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Azam FC utakuwa mgumu lakini tumejiandaa kuhakikisha tunapambana mpaka mwisho ili kuhakikisha tunapata alama tatu za ugenini.

Barker amesema ni wazi kuwa tunaenda kukutana na timu ngumu na msimu uliopita tulipata alama moja tu tulivyokutana hivyo tumejipanga kuhakikisha tunajituma kwa asilimia zote 100 ili kuweza kushinda.

Kuhusu hali ya kikosi, Barker amesema maandalizi ya mchezo yanaendelea vizuri na wachezaji wapo kwenye hali nzuri na tayari kwa mchezo wa kesho.

Advertisement

"Msimu uliopita tulipata alama moja tu dhidi ya Azam, na hiyo ilikuwa ni miongoni mwa changamoto kwenye mbio zetu za ubingwa ingawa tumeanza Ligi vizuri na malengo yetu ni kupata alama zote tatu kutoka kwao na tunajua haitakuwa rahisi lakini tupo hapa kupambana ili kufanikisha hilo," amesema Barker.

Kwa upande wake mlinzi wa kulia Nathaniel Chilambo amesema wao kama wachezaji wamejiandaa kujitoa kwa asilimia zote ili kuweza kupata alama tatu ingawa amekiri haitakuwa rahisi kutokana na ubora wa wapinzani.

"Sisi kama wachezaji tumejipanga kuhakikisha tunashinda, tunafahamu tunaenda kukutana na timu ambayo ina wachezaji imara na kocha bora pia hivyo haitakuwa mechi nyepesi lakini tunaahidi kutoa asilimia zote ili kupata alama tatu," amesema Chilambo.