Simba Sports Club

Timu yafanya Mazoezi ya mwisho Gymkhana

15 Sep 2026

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Gymkhana tayari kwa mchezo wa kesho wa Ligi Kuu NBC dhidi ya Azam FC.

Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na wapo kwenye hali nzuri tayari kwa mchezo huo ambao tunataraji utakuwa mgumu.

Advertisement

Morali za wachezaji zipo juu na kila mchezaji ambaye atapata nafasi kwenye mchezo wa kesho atakuwa tayari kujitoa kwa asilimia 100 kuipigania nembo ya klabu.

Mchezo wetu dhidi ya Azam utapigwa katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi saa moja usiku