Simba Sports Club

Tupo tayari kumalizia kazi tuliyoianza Malawi

13 Sep 2026

Leo saa 10 jioni kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kuikabili Mighty Wanderers katika mchezo wa marudiano wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Tutaingia uwanjani kwenye mchezo wa leo tukiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao moja tuliopata wiki iliyopita katika Uwanja wa Taifa wa Bingu nchini Malawi.

Tuna historia nzuri na timu kutoka Malawi......

Septemba 10/2022 tulicheza na Nyasa Big Bullets ya Malawi katika Ligi ya Mabingwa Afrika katika Uwanja wa Taifa wa Bingu na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 yaliyofungwa na John Bocco na Moses Phiri.

Mchezo wa marudiano ulipigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Septemba 18/2022 tuliibuka pia na ushindi wa mabao 2-0 ambayo yote yalifungwa na Moses Phiri.

Hali ya Kikosi....

Kiungo mshambuliaji, Libbase Gueye ambaye alikosekana katika mchezo uliopita amerejea kikosini baada ya kumaliza kutumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyopata msimu uliopita dhidi ya Petro De Luanda ya Angola.

Advertisement

Tutaendelea kuwakosa Nickson Kibabage na Shomari Kapombe ambao bado ni majeruhi.

Wachezaji wengine wote waliopo kikosini wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo ambapo kocha mkuu Steve Barker na wasaidizi wake watakuwa na wigo mpana wa kupanga kikosi.

Wachezaji wakuchungwa.....

Libbase Gueye, Anicet Oura, Elie Mpanzu na Clatous Chama ni nyota ambao wanatarajiwa kuwa mwiba mchungu kwa safu ya ulinzi ya Mighty Wanderers kwenye mchezo wa leo.

Matarajio ya jinsi mechi itakavyokuwa......

Mchezo unatarajiwa kuwa wakuvutia kutokana na aina ya soka kwa pande zote lakini historia inatubeba zaidi kila tunapocheza nyumbani kwenye michuano hii ya Ligi ya Mabingwa Afrika.