Leo saa 10 jioni kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kuikabili Mighty Wanderers katika mchezo wa marudiano wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kocha Mkuu Steve Barker amefanya mabadiliko ya wachezaji wawili ukilinganisha na kikosi kilichoanza mechi iliyopita nchini Malawi.
Barker amewaanzisha Libbase Gueye na Clatous Chama wakichukua nafasi za Kaletso Makgalwa na Ibraheem Jabaar.
Hiki hapa kikosi kamili kilichopangwa:
Djibrilla Kassali (39), Nathaniel Chilambo (26), Anthony Mligo (5), Ismail Toure (25), Rushine De Reuck (23), Yusuph Kagoma (21), Libbase Gueye (7), Neo Maema (35), Elie Mpanzu (34), Clatous Chama (17), Anicet Oura (20).
Wachezaji wa Akiba:
Hussein Abel (28), David Kameta Duchu (15), Vedastus Masinde (4), Ibraheem Jabaar (8), Morice Abraham (18), Ibrahim Doumbia (29), Ismail Mgunda (36), Inno Loemba (10), Keletso Makgalwa (11).