Leo saa moja usiku kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam kuikabili Mashujaa FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2026/2027.
Ni mchezo mgumu ambao tunataraji utakuwa mgumu hasa kutokana na ubora wa wapinzani wetu lakini tumejiandaa kuhakikisha tunapata alama tatu.
Nafasi za timu zote kwenye msimamo....
Tupo nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC tukiwa na alama 21 na mabao 13 baada ya kupata ushindi kwenye michezo yote saba tuliyocheza tukiwa na ushindi wa asilimia 100.
Kwa upande wapinzani wetu Mashujaa wapo nafasi ya nne kwenye msimamo wakiwa na alama 12 baada ya kucheza mechi saba.
Tulivyokutana mara ya mwisho....
Mara ya mwisho tulivyokutana na Mashujaa ilikuwa Aprili 14 mwaka huu kwenye mchezo wa mzunguko wa pili ambapo tuliibuka na ushindi wa mabao 3-0.
Mchezo huo ulipigwa katika Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma mabao yetu yalifungwa na Clatous Chama aliyefunga mawili na Seleman Mwalimu.
Hali za Kikosi.....
Kocha mkuu, Steve Barker ameweka wazi kuwa wachezaji wote hata waliokuwa majeruhi kama Wilson Nangu na Abdulazak Hamza wamefanya mazoezi kamili na wenzao na wapo tayari.
Wachezaji wakuchungwa.....
Libbase Gueye, Anicet Oura, Elie Mpanzu na Clatous Chama ni nyota ambao wanatarajiwa kuwa mwiba mchungu kwa safu ya ulinzi ya Mashujaa kwenye mchezo wa leo.
Kwa upande wapinzani wetu nyota wao wa kuchungwa ni Mishamo Daud, Michael Joseph na Haruna Chanongo.