Simba Sports Club

Timu yafanya Mazoezi ya mwisho Mo Arena

12 Oct 2026

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Mo Simba Arena tayari kwa mchezo wa kesho wa Ligi Kuu NBC dhidi ya Mashujaa FC utakaopigwa katika dimba la Uhuru, Dar es Salaam.

Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na wapo kwenye hali nzuri tayari kwa mchezo huo ambao tunataraji utakuwa mgumu.

Advertisement

Morali za wachezaji zipo juu na kila mchezaji yupo tayari hasa ukizingatia tumetoka kushinda mchezo wa Dabi ya Kariakoo.