Simba Sports Club

Tumemchakaza Mashujaa bila huruma

13 Oct 2026

Kikosi chetu kimefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao 6-1 dhidi ya Mashujaa FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Mchezo ulianza kwa kasi ya kawaida huku tukimiliki sehemu kubwa na kufika zaidi lango mwa Mashujaa ambao muda wote walikuwa nyuma wakizuia.

Libase Gueye alitupatia bao la kwanza dakika ya 16 kwa shuti kali la mguu wa kushoto nje ya 18 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Neo Maema.

Elie Mpanzu alitupatia bao la pili dakika ya 33 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Yusuph Kagoma.

Anicet Oura alitupatia bao la tatu dakika ya 54 baada ya kupokea mpira wa krosi uliopigwa na Libase.

Mpanzu alitupatia bao la nne dakika ya 58 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Morice Abraham.

Morice alitupatia bao tano dakika ya 60 baada ya kupokea mpira wa krosi uliopigwa na Mpanzu.

Advertisement

Seleman Bwenzi aliwapatia Mashujaa bao la kwanza dakika ya 63 kwa shuti kali nje ya 18 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Crispin Ngushi.

Ismail Toure alitupatia bao la sita dakika ya 69 kwa shuti kali la chini chini la mguu wa kushoto baada ya kupokea pasi Ibraheem Jabaar.

Ushindi huu unatufanya kufikisha alama 24 baada ya kushinda mechi zote nane tukiwa kilele mwa msimamo.

X1: Kassali, Chilambo, Mligo, Toure, Kagoma, Jabaar, Guaye (Makgalwa 65'), Maema (Morice 45') Mpanzu (Doumbia 65'), Chama (Mgunda 65') Oura (Msimu 78')

Walioonyeshwa kadi:

X1: Malika, Lyawatwa, Mwakinyuke (Bwenzi 60'), Mangalo, Madeleke, Mgandila (Balama 45'), Ngushi (Mundhir 87'), Tatiq (Kakoko 70') Michael (Mishamo 45'), Shamte, Kabunda

Walioonyeshwa kadi: Mwakinyuke 31' Kabunda 45+4' (Nyekundu) Shamte 75'