Leo saa 10 jioni kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa Taifa wa Bingu, Lilongwe nchini Malawi kuikabili Mighty Wanderers katika mchezo wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Tutaingia uwanjani kwenye mchezo wa leo tukiwa na lengo moja la kuhakikisha tunapambana ili kupata matokeo chanya yatakayo tusaidia kuvuka kwenye hatua hii.
Msimu uliopita kwenye michuano ya Afrika....
Msimu wa 2025/2026 tulishiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na tuliishia hatua ya makundi.
Kwa upande wa Mighty Wanderers wao walitolewa hatua ya awali kwa mikwaju ya penati 7-6 na Jwaneng Galaxy ya Botswana.
Tulivyokutana mara ya mwisho na timu kutoka Malawi......
Septemba 10/2022 tulicheza na Nyasa Big Bullets ya Malawi katika Ligi ya Mabingwa Afrika katika Uwanja wa Taifa wa Bingu na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 yaliyofungwa na John Bocco na Moses Phiri.
Mchezo wa marudiano ulipigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Septemba 18/2022 tuliibuka pia na ushindi wa mabao 2-0 ambayo yote yalifungwa na Moses Phiri.
Hali ya Kikosi....
Kiungo mshambuliaji, Libbase Gueye atakosekana kwenye mchezo wa leo kutokana na kutumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyopata msimu uliopita dhidi ya Petro De Luanda ya Angola.
Nyota wetu, Ibraheem Jabaar na Anthony Mligo ambao wamekosekana katika mechi zetu mbili za ligi zilizopita kutokana na kutumikia kadi nyekundu wote wapo tayari kuitumikia timu leo.
Wachezaji wengine wote 22 tuliosafiri nao kuja Malawi wapo tayari kwa ajili ya mchezo.
Wachezaji wakuchungwa.....
Anicet Oura, Elie Mpanzu na Clatous Chama ni nyota ambao wanatarajiwa kuwa mwiba mchungu kwa safu ya ulinzi ya Mighty Wanderers kwenye mchezo wa leo.
Matarajio ya jinsi mechi itakavyokuwa......
Mchezo unatarajiwa kuwa wakuvutia kutokana na aina ya soka kwa pande zote lakini historia inatubeba zaidi kila tunapokutana na timu kutoka Malawi.