Leo saa 10 jioni kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa Taifa wa Bingu, Lilongwe nchini Malawi kuikabili Mighty Wanderers katika mchezo wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kocha Mkuu, Steve Barker amefanya mabadiliko ya wachezaji wanne ukilinganisha na kikosi kilichoanza mechi iliyopita ya Ligi Kuu dhidi ya Geita Gold.
Barker amewaanzisha, Anthony Mligo, Yusuph Kagoma, Kaletso Makgalwa na Ibraheem Jabaar wakichukua nafasi za Hussein Mbegu, Morice Abraham, Libbase Gueye na Clatous Chama.
Hiki hapa kikosi kamili kilichopangwa:
Djibrilla Kassali (39), Nathaniel Chilambo (26), Anthony Mligo (5), Ismail Toure (25), Rushine De Reuck (23), Yusuph Kagoma (21), Keletso Makgalwa (11), Ibraheem Jabaar (8), Elie Mpanzu (34), Neo Maema (35), Anicet Oura (20).
Wachezaji wa Akiba:
Hussein Abel (28), David Kameta Duchu (15), Vedastus Masinde (4), Inno Loemba (10), Bakari Msimu (19), Ibrahim Doumbia (29), Ismail Mgunda (36), Clatous Chama (17), Morice Abraham (18),