Simba Sports Club

Tumepata ushindi mbele ya Mighty Wanderers

6 Sep 2026

Mchezo wetu wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mighty Wanderers uliopigwa Uwanja wa Taifa wa Bingu nchini Malawi umemalizika kwa ushindi wa bao moja.

Mchezo ulianza kwa kasi ya kawaida huku timu zote zikicheza kwa tahadhari lakini dakika 15 za mwanzo tulilifikia zaidi lango la Might Wonderers.

Dakika 45 za mwanzo mpira ulichezwa zaidi katikati ya uwanja huku safu zote za ulinzi zikihakikishwa kipa wao hafikiwi kirahisi.

Anicet Oura alitupatia bao hilo pekee dakika ya 65 baada ya mlinzi wa kati Emmanuel Nyirenda kuokoa mpira kabla ya kumkuta mfungaji.

Baada ya bao hilo tuliendelea kushambuliana kwa zamu lakini hata hivyo pamoja na mashambulizi yote matokeo hayakuweza kubadilika.

Advertisement

Mchezo wa marudiano utapigwa jijini Dar es Salaam Septemba 13 na mshindi wa jumla atatinga moja kwa moja hatua ya kwanza ya michuano hii.

X1: Khungwa, Sanubi, Nyirenda, Ng'ambi, Silwimba, Singini, Kamanga, Kudonto Jr (Adam 71') Kaliati (Mithi 86'), Chirwa, Sulumba (Sama 67')

Walioonyeshwa kadi: Nyirenda 82'

X1: Kassali, Chilambo, Mligo, Toure, De Reuck, Kagoma, Makgalwa (Morice 71'), Jabaar (Chama 61') Mpanzu (Doumbia 61'), Maema, Oura

Walioonyeshwa kadi: Toure 40'