Simba Sports Club

Hivi hapa Viingilio vya mechi ya marudiano dhidi ya Mighty Wanderers

10 Sep 2026

Mchezo wetu wa marudiano wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mighty Wanderers utapigwa Jumapili Septemba, 13 katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam saa 10 jioni.

Tumeweka wazi viingilio vya mchezo huo na tayari tiketi zimeanza kuuzwa kwa njia ya mitandao ya simu pamoja na N CARD.

Kiingilio cha chini itakuwa kama kawaida Shilingi 5000 ili kuweza kuwawezesha mashabiki kujitokeza kwa wingi kuja kuipa sapoti timu yetu.

Hivi hapa Viingilio kamili vilivyotangazwa:

Advertisement

Mzunguko Shilingi 5000

VIP Shilingi 30,000

Platinum Shilingi 150,000.

Pia unaweza kupata tiketi yako kupitia mtandao wa jamiipay.kimtandao.co.tz