Tumefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao 6-1 dhidi ya FC 15 De Agosto kutoka Equatorial Guinea katika mchezo mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Tulianza mchezo kwa kasi huku tukiwafikia zaidi 15 De Agosto na kufanya mashambulizi ingawa ufanisi wa kutumia nafasi tulizopata haukuwa mzuri.
Nathaniel Chilambo alitupatia bao la kwanza kwa kichwa dakika ya 43 baada ya shuti lililopigwa na Elie Mpanzu kuzuiliwa na walinzi kabla ya kumkuta mfungaji.
Elie Mpanzu alitupatia bao la pili dakika ya 56 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Libase Gueye.
Ibrahim Doumbia alitupatia bao la tatu dakika ya 64 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa mlinzi wa kushoto, Anthony Mligo.
Kaletso Makgalwa alitupatia bao la nne dakika ya 71 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Morice Abraham.
Anicet Oura alitupatia bao la tano dakika ya 82 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na winga, Bakari Msimu.
Doumbia alitupatia bao la sita dakika ya 87 akiwa ndani ya 18 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Abraham.
Alozie Uwandu aliwapatia De Agosto bao la kufuatia machozi dakika ya 90 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Enrique Engono.
Mchezo wetu wa marudiano utakapigwa Jumapili Oktoba 24 katika Uwanja wa Uhuru saa 10 jioni.
X1: Awono, Antonio, Verseau, Christ ( Uwandu 45') Enrique, Mamadou (Obongo 45), Miguel, Gabriel, Ndiye, Thierry, Aston
Walioonyeshwa kadi: Mamadou 27' Antonio 48'
X1: Kassali, Chilambo, Mligo, Toure, De Reuck, Kagoma (Jabaar 68') Gueye (Msimu 75') Maema (Morice 68'), Mpanzu (Doumbia 60') Chama (Makgalwa 60'), Oura
Walioonyeshwa kadi: Rushine 73'