Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam tayari kwa mchezo wa kesho wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC 15 De Agosto kutoka Equatorial utakaoanza saa tisa Alasiri.
Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na wapo kwenye hali nzuri tayari kwa mchezo huo ambao tunataraji utakuwa mgumu.
Nahodha wetu, Shomari Kapombe ambaye hajacheza mechi yoyote msimu huu kutokana nakuwa majeruhi pamoja na mlinzi wa kati, Wilson Nangu wameshiriki mazoezi hayo na wapo fiti asilimia 100 tayari kwa mchezo wa kesho.