Kikosi chetu kimeendelea na mazoezi katika Uwanja wa Mo Simba Arena kujiandaa na mchezo wa hatua ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC 15 De Agosto kutoka Equatorial Guinea.
Mchezo dhidi ya 15 De Agosto utapigwa katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam siku ya Jumatano, Oktoba 21 saa tisa Alasiri.
Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na wapo kwenye hali nzuri huku morali zao zikiwa juu.