Tulianza mchezo kwa kasi huku tukifika zaidi langoni mwa Mafunzo na kutengeneza nafasi lakini walinzi wao walikuwa imara.
Katika dakika zote 45 za kipindi cha kwanza Mafunzo walikuwa wakicheza kwa kuzuia huku wakifanya mashambulizi machache ya kushtukiza.
Seleman Mwalimu alitupatia bao la kwanza dakika ya 53 kwa shuti kali akiwa ndani ya 18 baada ya walinzi wa Mafunzo kuzembea kuondoa hatari.
Advertisement
Matokeo haya yanatufanya kukutana na timu ya Mlandege katika mchezo wa nusu fainali utakaopigwa siku ya Jumapili katika Uwanja wa New Amaan Zanzibar.
X1: Abel, Duchu, Mligo, Masinde, Mbegu, Semfuko, Chasambi (Bajaber 45') Loemba (Kante 59'), Mwangosi (Mwalimu 45'), Morice (Chama 65'), Kibaila (Gueye 65')
Waliionyeshwa kadi: Mbegu 23'