Mchezo huo ambao tunategemea utakuwa mgumu na wenye upinzani mkubwa utapigwa kesho katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo kikamilifu na wapo tayari kuhakikisha wanapambana mpaka mwisho ili kuhakikisha alama tatu zinabaki nyumbani.
Advertisement
Simba Queens itaingia kwenye mchezo wa kesho ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 2-0 iliyopata dhidi ya Fountain Gate Princess siku ya Jumatano.