Matokeo ya mabao 3-0 tuliyopata katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC 15 De Agosto kutoka Equatorial Guinea yametuwezesha kutinga hatua ya makundi.
Wapinzani wetu 15 De Agosto walianza mchezo kwa kasi huku wakionekana kufika zaidi langoni kutafuta bao la mapema katika dakika 15 za mwanzo lakini hata hivyo tulikuwa watulivu kuondoa hatari zote.
Kuanzia dakika 15 kulirejesha umiliki wa mchezo na kufanya mashambulizi mengi langoni mwa De Agosto lakini umakini kwenye kutumia nafasi haukuwa na ufanisi wa asilimia 100.
Anicet Oura alitupatia bao la kwanza dakika ya 56 kwa shuti kali nje ya 18 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Kaletso Makgalwa.
Elie Mpanzu alitupatia bao la pili dakika ya 68 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Oura.
Makgalwa alikamilisha karamu ya mabao kwa kutupatia bao la nne dakika ya 76 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Nathaniel Chilambo.
Matokeo haya yanatufanya kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya mabao 9-1.
X1: Kassali, Duchu, Kibabage (Chilambo 60'), Nindi, De Reuck (Toure 45') Jabaar, Guaye (Oura 60'), Morice (Loemba 64'), Doumbia (Mpanzu 58'), Chama, Makgalwa
Walioonyeshwa kadi: Oura 70'
X1: Awono, Antonio, Verseau, Christ, Enrique, Mamadou, Miguel, Gabriel, Ndiye, Thierry, Aston
Walioonyeshwa kadi: Zanga 21' Antonio 80'
[18:13, 25/10/2026] Kagoma: Highlights: Simba 3-0 FC 15 De Agosto