Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Mo Simba Arena tayari kwa mchezo wa kesho wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC 15 De Agosto kutoka Equatorial utakaoanza saa 10 jioni.
Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na wapo kwenye hali nzuri tayari kwa mchezo huo ambao tunataka kupata mabao mengi ili kuweka historia ya kufuzu hatua ya makundi kwa kishindo zaidi
Morali za wachezaji zipo juu na kila mchezaji yupo tayari hasa ukizingatia tutakuwa nyumbani na kupata sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki wetu.