Simba Sports Club

Doumbia Mgeni Rasmi Jumapili

22 Oct 2026

Mshambuliaji wetu, Ibrahim Doumbia atakuwa mgeni rasmi katika mchezo wetu wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC 15 De Agosto kutoka Equatorial Guinea utakaopigwa Jumapili saa 10 jioni Uwanja wa Uhuru.

Meneja Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally amesema tumeamua kumpa heshima Doumbia kutokana na uwezo aliounyesha kwenye mchezo wa jana ambapo alifunga mabao mawili kwenye ushindi wa 6-1.

Ahmed ameongeza kuwa watu wengi walimkatia tamaa na kumtupia maneno machafu kwenye mitandao ya jamii ndio maana tumeamua kumpa heshima yake anayostahili.

"Doumbia ndiye mgeni rasmi wa mchezo wetu wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi 15 De Agosto na lengo ni moja tu kumpa thamani anayostahili," amesema Ahmed.

Ahmed amewatangaza pia waamuzi wa mchezo huo ambapo watatoka nchini DR Congo kama ifuatavyo:

Mwamuzi wa kati, Jean Jacques Ndala

Advertisement

Msaidizi namba 1, Guylain Bongele Ngila

Msaidizi namba 2, Mwanya Gradel Mbilizi

Mwamuzi wa Akiba, Masangune Louis Mwamba

Kamishna wa mchezo, Mutwakkil Abbas Mohamed kutoka Sudan

Msamamizi wa waamuzi, Bruno Tembo kutoka Zambia.