Simba Sports Club

Tumeshinda nyumbani mbele ya Geita

31 Aug 2026

Tumefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo.

Clatous Chama alitupatia bao kwanza dakika ya 21 akiwa ndani ya 18 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Libasse Gueye.

Baada ya bao hilo tuliendelea kufanya mashambulizi mengi langoni mwa Geita lakini tulikosa umakini wa kuzitumia nafasi tulizopata huku wapinzani wakifanya mashambulizi machache ya kushtukiza.

Libbase Gueye alitupatia bao la pili dakika ya 58 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na mlinzi, Nathaniel Chilambo.

Ushindi huu unatufanya kufikisha alama 15 baada ya kushinda mechi zetu zote tano tukiwa nafasi ya pili kwenye msimamo tukizidiwa mabao yakufunga na wanaoongoza.

Advertisement

X1: Kassali, Mbegu, Chilambo, Toure, De Reuck, Maema (Loemba 80'), Gueye (Doumbia 61'), Morice (Kagoma 61'), Mpanzu (Msimu 75'), Chama, Oura (Makgalwa 75')

Walioonyeshwa kadi: Morice 57'

X1: Faustine, Kigi, Datius, Med, Ali Ali, Kulandana, Omary (Kuzoza 76') Ng'ondya (Ismail 76'), Kassim (Kaboma 60') Maulid (Bunyenze 87'), Chirwa (Vincent 61')

Walioonyeshwa kadi: Chirwa 12' Kassim 23'