Simba Sports Club

Alichosema kocha Barker kuelekea mchezo dhidi ya Geita Gold

30 Aug 2026

Kocha Mkuu, Steve Barker amesema maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Geita Gold utakaopigwa kesho saa 12:30 jioni katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo yamekamilika.

Barker amesema tunajua tunaenda kukutana na timu imara ambayo ipo kwenye kiwango bora kwa sasa yenye wachezaji wenye uwezo mkubwa pamoja na kocha bora lakini tupo tayari kuwakabili.

Barker ameongeza kuwa lengo letu ni kucheza soka safi na kupata alama tatu ili kuendelea kubaki kwenye nafasi za juu katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.

"Tuna changamoto ya majeruhi kwenye kikosi chetu lakini tumewaandaa wachezaji waliopo kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya Geita Gold, haitakuwa mechi rahisi lakini tupo kupambana ili tuweze kupata ushindi."

Advertisement

"Tunafahamu tunaenda kukutana na timu ngumu ambayo ina wachezaji bora na pia wana kocha mzuri lakini kwa maandalizi tuliyofanya tuna nafasi kubwa ya kupata alama tatu nyumbani," amesema kocha Barker.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji kiungo mkabaji, Daud Semfuko amesema kila mmoja yupo tayari kuhakikisha anapambana mpaka mwisho kuhakikisha anaisaidia timu kupata ushindi ingawa haitakuwa kazi rahisi.

"Kwa upande wetu wachezaji tupo tayari kufuata maelekezo tutakayopewa na walimu ili kuweza kupata alama tatu muhimu nyumbani ikiwa ndio lengo letu kuu," amesema Semfuko.