Simba Sports Club

Tumerejea tena Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo

24 Aug 2026

Meneja Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally ametangaza rasmi mechi zetu zote nyumbani za Ligi Kuu ya NBC pamoja na CRDB Federation Cup zitafanyika katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo.

Ahmed amesema awali tulitangaza kutumia Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam lakini kutokana na bado kuwa kwenye matengenezo tumerejea Meja Jenerali Isamuhyo.

Ahmed amesema Uwanja wa Meja Isamuhyo umetupa mafanikio makubwa msimu uliopita na tunataraji tutaendelea kufanya vizuri.

Advertisement

Ahmed ameongeza kuwa mchezo wetu wa kwanza wa nyumbani dhidi ya Coastal Union utakaopigwa Alhamisi Agosti 27 utachezwa Meja Jenerali Isamuhyo.

"Naomba niwatangazie rasmi kuwa mechi zetu za nyumbani tutacheza katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo na tutaanza dhidi ya Coastal Union siku ya Alhamisi," amesema Ahmed.