Simba Sports Club

Tumepoteza mchezo dhidi ya Sekhukhune United

3 Oct 2026

Mchezo wetu wa kirafiki wa kiufundi dhidi ya Sekhukhune United uliopigwa katika jiji la Johannesburg nchini Afrika Kusini umemalizika kwa kupoteza kwa mabao 2-1.

Chibuike Ohizu aliipatia Sekhukhune bao la mapema dakika ya pili baada ya shambulizi la kushtukiza ambalo liliwakuta walinzi wetu wakiwa bado hawajajipanga.

Baada ya bao hilo tuliamka na kuliandama lango la Sekhukhune na kutengeneza nafasi kadhaa ambazo hata hivyo hatukuweza kuzitumia.

Elie Mpanzu alitupatia bao la kusawazisha dakika 40 baada ya kuunganisha mpira wa krosi uliopigwa na Nickson Kibabage.

Kipindi cha pili kila timu ilirejea kwa kasi na kufanya mashambulizi kwa zamu huku mpira ukichezwa zaidi katikati ya uwanja.

Advertisement

Sekhukhune walipata bao la pili dakika ya 74 baada ya mchezaji wao kuwazidi ujanja walinzi wetu.

Dakika ya 87 Kelvin Nashon alifunga bao lakini mwamuzi alilikataa baada ya kutafsiri kuwa Neo Maema alifanya madhambi kabla ya kumkuta mfungaji na kutufanya kumaliza mchezo kwa kupoteza.

Mchezo wa leo umekamilisha rasmi kambi yetu ya mazoezi ya siku nchini Afrika Kusini ambao kesho kikosi kitarejea jijini Dar es Salaam kuendelea na maandalizi ya mchezo wa Dabi ya Kariakoo.

X1: Abel, Duchu, Kibabage, De Rueck (Semfuko), Toure (Nindi), Kagoma (Jabaar), Guaye (Bashir), Maema, Mpanzu (Mgunda), Chama, Oura (Makgalwa)