Kikosi chetu kimerejea jijini Dar es Salaam kutoka nchini Afrika baada ya kukamilisha kambi ya siku 10 ya maandalizi.
Baada ya kufika jijini Dar es Salaam kikosi kimeingia kambini moja kwa moja kujiandaa na mchezo wa Dabi ya Kariakoo utakaopigwa Jumamosi, Oktoba 10.
Kikiwa nchini Afrika Kusini kikosi chetu kilifanikiwa kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Polokwane City na Sekhukhune United.
Nyota waliokuwa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' nao watajiunga na timu mara tu watakapotua nchini kutoka Morocco.