Mchezo wetu wa kirafiki Kimataifa wa kilele cha Simba Day dhidi ya Polisi Kenya uliopigwa Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam umemalizika kwa kupoteza kwa bao moja.
Tulianza mchezo kwa kasi huku tukishambulia zaidi lango la Polisi Kenya lakini hatukuwa na ufanisi wa asilimia 100 kwenye kuzitumia nafasi tulizopata.
Polisi Kenya walicheza kwa kuzuia muda mwingi wakifanya mashambulizi machache dakika 45 za kipindi cha kwanza wakiwa hawajapiga shuti lililolenga lango.
Kipindi cha pili tulifanya mabadiliko ya wachezaji wote 11 walioanza na kusaidia kuongeza kasi kwenye eneo la ushambuliaji.
Hata hivyo Polisi Kenya wakiendelea kucheza soka la kukaa nyuma huku wakifanya mashambulizi machache ambayo hayakuwa na hatari.
Elvis Rupia aliwapatia Polisi Kenya bao hilo pekee dakika ya pili ya nyongeza kipindi cha pili baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa Egade.
X1: Kassali (Abel 45') Duchu (Chilambo 45'), Kibabage (Mligo 45') Toure (Semfuko 45' Mbegu 78'), De Reuck (Masinde 45 Kibaila 78'), Kagoma (Maema 32' Nashon 60'), Gueye (Msimu 45'), Jabaar (Loemba 45) Mpanzu (Doumbia 45'), Morice (Chama 45') Oura (Makgalwa 45')
Walioonyeshwa kadi:
X1: Ochieng, Edage, Briyock, Christophe, Ouma, Omondi, Esiye, Oliver (Ndoket 73'), Junior, Akwanyi (Quansah 73'), Ngava (Traore 59')
Walioonyeshwa kadi: Asante Kusi 87'