Simba Sports Club

Timu imeondoka kuelekea Zanzibar

10 Aug 2026

Kikosi chetu kimeondoka alfajiri hii kwa kuelekea Zanzibar tayari kwa mchezo wa Ngao ya Jamii utakaopigwa Jumatano saa mbili na nusu usiku Uwanja wa New Amaan.

Kikosi kimeondoka na jumla ya wachezaji 26 tayari kwa mchezo huo ambao utakuwa dhidi ya watani wetu wa jadi Yanga.

Advertisement

Jana jioni kikosi kimefanya mazoezi ya gym kujiweka sawa baada ya mchezo wa juzi dhidi ya Polisi Kenya kwenye kilele cha Simba Day.

Leo jioni kikosi kitafanya mazoezi ya kwanza Zanzibar na Jumanne kitafanya ya mwisho kabla ya Jumatano kushuka dimbani.