Mchezo wetu wa Ngao ya Jamii dhidi ya watani wetu wa jadi Yanga uliopigwa Uwanja wa New Amaan Zanzibar umemalizika kwa kupoteza kwa bao moja.
Mchezo ulianza kwa kasi ya kawaida huku tukimiliki sehemu kubwa katika dakika 20 za kwanza tukifanya mashambulizi kadhaa lakini hayakuwa ya madhara makubwa langoni kwa Yanga.
Albert Kangwanda aliipatia Yanga bao la kwanza kwa kichwa dakika ya 31 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Shadrack Boka.
Kipindi cha pili Yanga walirudi wakiwa bora na walimiliki sehemu kubwa dakika 20 za mwanzo lakini tulikuwa imara kwenye kuzuia.
X1: Diara, Yao, Boka, Mwamnyeto, Bacca, Abuya, Kangwanda (Zimbwe Jr'), Mudathir, Shalulile (Okello 86'), Nzengeli, Zakouani (Toure 45')
Walioonyeshwa kadi: Abuya 6' Bacca 45+2' Nzengeli 55' Boka 81' Yao 90+5'
X1: Kassali, Duchu, Kibabage (Mligo 77'), Toure, De Reuck, Kagoma (Morice 86'), Gueye (Msimu 77'), Jabaar, Doumbia (Mpanzu 45'), Chama (Makgalwa 56'), Oura
Walioonyeshwa kadi: Jabaar 43' Oura 53' Mligo 95+5'