Simba Sports Club

Kikosi kinachoanza dhidi ya Yanga

12 Aug 2026

Leo saa 2:30 usiku tutacheza mchezo wa Ngao ya Jamii kuashiria kufunguliwa kwa pazia la Ligi Kuu msimu wa 2026/2027 dhidi ya Yanga katika Uwanja wa New Amaan Zanzibar.

Kocha mkuu, Steve Barker amefanya mabadiliko ya wachezaji wawili ukilinganisha na kikosi kilichoanza mechi iliyopita dhidi ya Polisi Kenya kwenye Tamasha la Simba Day.

Barker amewaanzisha Clatous Chama na Ibrahim Doumbia wakichukua nafasi za Morice Abraham na Elie Mpanzu.

Advertisement

Hiki hapa kikosi kamili kilichopangwa:

Djibrilla Kassali (39), David Kameta Duchu (15), Nickson Kibabage (3), Ismail Toure (25), Rushine De Reuck (23), Yusuph Kagoma (21), Libbase Gueye (7), Ibraheem Jabaar (8), Ibrahim Doumbia (29), Clatous Chama (17), Anicet Oura (20).

Wachezaji wa Akiba:

Hussein Abel (28), Nathaniel Chilambo (26), Anthony Mligo (5), Vedastus Masinde (4), Daud Semfuko (37), Bakari Msimu (19), Inno Loemba (10), Elie Mpanzu (34), Morice Abraham (18), Keletso Makgalwa (11).