Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa nje wa New Amaan Zanzibar tayari kwa mchezo wa kesho wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga.
Wachezaji wote 25 tuliosafiri nao kuja Zanzibar wameshiriki mazoezi hayo na hakuna aliyepata maumivu ambayo yatamfanya kuikosa mechi ya kesho.
Kocha mkuu, Steve Barker ameweka wazi kuwa tutaingia kwenye mchezo wa kesho kwa lengo moja la kuhakikisha tunashinda na kuchukua Ngao ya Jamii.
Mara ya mwisho kutwaa Ngao ya Jamii ilikuwa Agosti, 2023 tulipoifunga Yanga katika Uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Tanga.