Leo asubuhi kikosi chetu kimecheza mechi ya kirafiki ya Kimataifa dhidi ya El Merreikh ya Sudan uliopigwa jijini Kigali nchini Rwanda na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Mchezo huo ambao ni wa mwisho kwa timu kucheza ikiwa Kigali, Rwanda ulikuwa mzuri huku timu zikishambuliana kwa zamu.
Libbase Gueye alitupatia bao la kwanza dakika ya tatu baada ya kupokea pasi safi kutoka Kaletso Makgalwa.
Baada ya bao hilo timu zote ziliendelea kushambuliana kwa zamu huku safu zote za ulinzi zikiwa imara.
Ibrahim Doumbia alitupatia bao la pili muda mfupi baada ya kuingia kipindi cha pili baada ya kupokea pasi kutoka kwa Morice Abraham.
Baada ya mchezo wa leo hakuna tena programu ya mazoezi itakayoendelea na kesho kitaanza safari ya kurejea jijini Dar es Salaam.
Hiki hapa kikosi kamili kilichopangwa:
Kassali (Alex), Chilambo (Duchu), Kibabage (Mligo), Toure (Vedastus), De Reuck (Semfuko), Kagoma (Loemba), Gueye (Bakari), Jabaar (Nashon), Mpanzu (Doumbia), Morice (Oura) Keletso