Simba Sports Club

Queens yaibuka na ushindi dhidi ya Zesco Girls

5 Aug 2026

Kikosi chetu cha Simba Queens kimecheza mchezo wa kirafiki wa Kimataifa dhidi ya Zesco Ndola Girls na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mtanange uliopigwa KMC Complex, Dar Es Salaam.

Mchezo huo ulikuwa mkali huku kila timu ikitumia mbinu zaidi ili kuweza kupata matokeo chanya lakini Queens walikuwa bora kwenye maeneo mengi.

Hellen Kutsanedzi alitupatia bao la kwanza mapema kipindi cha kwanza kwa shuti kali nje ya 18 lililomshinda mlinda mlango wa Zesco Girls.

Advertisement

Kipindi cha pili Elizabeth Wambui alitupatia bao la pili baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Senaf Demise.

Simba Queens itacheza mechi nyingine ya kirafiki siku ya Jumamosi ya Agosti 8 katika kilele cha Simba Day ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya msimu.

Simba Queens inaendelea na maandalizi ya michuano ya CECAFA Women's Champions League Qualifiers itakayofanyika baadae mwezi huu Kigali nchini Rwanda.