Droo ya hatua ya awali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika imepangwa mchana wa leo jijini Cairo nchini Misri na tumepangwa na Might Wonderers ya Malawi.
Mchezo wa kwanza utakuwa ugenini nchini Malawi kati ya Septemba 4-6 na mechi ya marudiano itakuwa kati ya Septemba 11-13 jijini Dar es Salaam.
Advertisement
Mshindi kati yetu dhidi ya Might Wonderers atakutana na mshindi kati ya 15 De Agosto ya Equatorial Guinea na Fomboni FC ya Comoro.
Mechi za kwanza hatua ya pili itapigwa Oktoba 16-18 wakati mechi ya marudiano itakuwa Oktoba 23-25.