Simba Sports Club

Timu yafanya mazoezi ya mwisho Rwanda

3 Aug 2026

Kikosi chetu leo kimefanya mazoezi ya mwisho kikiwa Kigali nchini Rwanda na kesho saa tano asubuhi kitacheza mechi ya kirafiki dhidi ya El Merreikh kutoka Sudan.

Baada ya mchezo wa kesho kikosi hakitakuwa na programu nyingine ya mazoezi badala yake kitarejea jijini Dar es Salaam, Jumatano Agosti 5 kuendelea na maandalizi ya Simba Day.

Advertisement

Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na wapo tayari kwa mchezo wa kesho na hakuna aliyepata maumivu ambayo yatamfanya kuikosa mechi hiyo.

Mchezo dhidi ya El Merreikh utahitimisha wiki mbili za maandalizi ya msimu wa mashindano 2026/2027 katika Jiji la Kigali nchini Rwanda kabla ya kurejea nyumbani kuendelea na ratiba nyingine.